islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


NEEMA YA PEPO NA ADHABU YA JAHANAM


9095
wasifu

mwenyezi mungu ameumba moto na akawaonya watu na huo moto wamuogope,na ameumba pepo na akawavutia watu ili wamtarajie yeye,kwani kumuogopa mwenyezi mungu kuna fanya moyo ufanye kila jema,na matumaini yanao muongoza mja kupata radhi za mwenyezi mungu na thawabu zake,na yana msukuma mja awe na hima ya kufanya matendo mema na yanamuepusha na matendo mabaya

Khutba ya

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Mwenye kurehemu wema na wabaya ulimwenguni, Mwenye kurehemu wema watupu kesho akhera. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Ambaye Ameumba pepo na moto. Mwenye kufanya wema atamlipa pepo, na Mwenye kufanya mabaya atamlipa moto. Na Swala na Salamu zimuende Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), na Maswahaba wake na Jamaa zake wote.

Nini neema? kila linalo takiwa na kupendeza huitwa neema. Lakini neema ya uhakika ni kufaulu Akhera na kuingia peponi. Pepo ni nyumba ilyo andaliwa watu wema ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), ndani kuna majumba na mashamba yaliyo na miti tofauti, na mito aina mbali mbali.

Enyi Waislamu leo tutazungumzia juu ya bidhaa iliyo ghali haipati bidhaa hiyo ila aliye rehemewa na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Wanaikimbilia biashara hiyo kila mmoja wetu sawa akiwa mume au mke, ni bidhaa iliyo na thamani kubwa inatafutwa na kila mtu. walienda mbio waliopita katika Waislamu na mpaka Waislamu wa sasa kwa lengo la kupata bidhaa hiyo. Na bidhaa hiyo si nyingine bali ni Pepo, iliyo andaliwa wale wote wenye vitendo vyema. Kama pepo ilivyo andaliwa kwa watu wema, vile vile Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) akauandaa moto kwa makafiri na wanafiki na kila anayemuasi Mwenyezi Mungu. Na pepo ni ya wanaomcha Mwenyezi Mungu, na moto ni ya wanaomuasi Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ) [آل عمران: 133]

{{Kimbilieni msamaha wa Mwenyezi Mungu na pepo upana wake ni mbingu na ardhi wameandaliwa wamchao Mwenyezi Mungu}} [Al-Imran:133].

Na Akasema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا وَلَنْ تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ) [البقرة: 24]

{{Na msipo fanya sasa na wala hamtofanya mbelini, ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na binidamu umeandaliwa makafiri}} [Al-Baqarah : 24].

Enyi Mlioamini, Hakika pepo ni nyumba ya wachaji Mungu. Nyumba iliyo neemeshwa imeandaliwa watu wema miongoni mwa Mitume na wa kweli na mashahidi pepo inayo pita chini yake mito, na nyumba ambazo kuta zake ni dhahabu na fedha, ndani yake mna wake wema walio wazuri, ndani yake watu wanakula wala hawaendi haja, kunao ndani ya pepo walio neemeshwa wana furaha siku zote wala hawapati huzuni wanacheka na wala hawalii watakuwa hai siku zote na wala hawatokufa. Nyuso zao zina furaha, ndani yake mna Hurul-‘Ain. Bali watu wa peponi wana neema zaidi na zaidi kwenye pepo mna mambo jicho halijaona wala sikio halijasikia. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

قال تعالى) : فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ )[السجدة: 17]

{{Haijui nafsi yaliyo fichwa katika hayo yanayo furahisha macho yao. Hayo ni malipo yale waliyo yafanya}} [Assajdah : 17].

Neema za Peponi katika Hadithi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

Na Hadithi nyingi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) zimebainisha hayo. Imepokewa na Abi Hurayra, Akipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Anasema: [ Mwenyezi Mungu ( alie mshindi na mwenye nguvu: Nime waandalia waja wangu neema ambao jicho halijaona na wala sikio halijasikia na wala haipiti fikra katika moyo wa mwanadamu]. Vile vile imekuja katika Hadithi za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Ameipokea Abu Hurayra Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hakika kundi la kwanza Litakaloingia peponi litaingia kama mwezi wa kumi na nne na wanaofuatia ni kama nyota iliyo mbinguni kwa muangaza wake hawakojoi wala hawaendi haja kubwa pafumu yao ni miski wake zao ni Hurul-‘Ain umbile lao ni moja kwa sura ya baba yao Adam dhiraa sitini kwenda juu]. Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Anayeingia peponi atastarehe wala hangonjeki, wala nguo yake hairaruki wala hawi mzee] (Muslim).

Vilevile katika kuonesha neema za peponi ni Hadithi ya Abu-Said Al-Khudhriyi na Abu Hurayrah wakipokea kwa Mume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema: [ Atalingania mwenye kulingania Aseme: Hakika uzima ni wenu na hamtakuwa wagonjwa kabisa, na hakika ni wenu nyinyi uhai hamtokufa kabisa, na hakika ni wenu nyinyi ubarobaro hamtakuwa wazee kabisa, na hakika ni zenu nyinyi starehe hamtakuwa na shida kabisa]. [ Na wataitwa waambiwe hiyo ndiyo pepo mlio ridhishwa ni malipo yale mliyoyafanya].

Baada ya kuzungumzia watu wa peponi na starehe zao. Kidogo tuizungumzie hali ya watu wa motoni na sifa zao na hali ya moto, ndani ya moto mna vinywaji vikali. Hakika moto ni nyumba ya watu wabaya, na ni nyumba ya adhabu kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : لَهُمْ شَرَابٌ مِنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ) [الأنعام: 70]

{{Ni za watu wa motoni vinywaji vya maji ya moto na adhabu yenye kuumiza kwa sababu ya kukanusha kwao}} [An-Aam : 70].

Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :

وقال تعالى أيضا) : وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ) [يونس: 4]

.

{{Na wale waliyo kufuru ni vyao wao vinywaji vikali na adhabu yenye kuumiza kwa walivyokuwa wamekufuru}} [Yuunus : 4].

Kwa hivyo, Moto ni mahali pa watu wabaya wanaokosea amri ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى : (هَذَا وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآَبٍ 55 جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ56) [ص55: 56]

{{Hivi basi hakika wapotevu wana mashukio mabaya, wataingia moto wa jahanamu na ubaya wa marudio ni kurudia motoni}} [Saad : 55—65].

Na katika kukamilisha kuizungumzia habari ya moto na sifa zake ni Hadithi Shaqiq. Imetokana na shaqiq amepokea kwa ‘Abdillahi Akisema: Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) : [Utaletwa moto siku hiyo umefungwa vifungo sabini elfu na kila kifungo kimoja kina vutwa na Malaika sabini elfu, wanauburuza] Tunamuomba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Atuepushe na moto wa Jahannam Atujaalie ni katika wenye kusikia mema pamoja na kuyafuata.

Khutba ya pili

Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu Aliye umba mbingu na ardhi pasina nguzo Aliye takasika na shirki na rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad na Sahaba zake pamoja na Jamaa zake walio wema. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى) : إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآَنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ )[التوبة: 111]

{{Hakika Mwenyezi Mungu Amenunuwa kwa waumini nafsi zao na mali yao kwa pepo. Wana pigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wanauwa na wanauawa}} [Tawba : 111].

Sababu za kupata pepo :-

Imani kamili iliyo kita ndani ya moyo

Kutenda vitendo vyema.

Kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

Kupigana Jihadi kwa ajili ya kutetea Dini ya Allah

Kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Kuwafanyia wema wazazi wawili.

Na ushahidi wa yote ni Hadith za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Imepokewa na Jarir Bin Abdillahi: tulikuwa na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), na ulikuwa mwezi wa kumi na nne, Mtume akawaambia: [ Hakika yenu mtamuona Mola wenu kama mnavyo uona mwezi kwa wazi hamtochoka. Mkiweza msishinde na kusali kabla ya kutoka juwa na kabla ya kuchwa]. Kwa maana isiwapite nyinyi Swala ya Asubuhi na Al-asri. Na neno lake Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Enyi watu peaneni salamu na mulishe chakula na muunge kizazi na mswali usiku na watu wamelala, mtaingia peponi kwa amani].

Kama ambavyo sababu hizi hukupelekea peponi hatuna budi kukuelezea sababu za kupelekea watu motoni.

Sababu za kukupelekea motoni nazo ni:-

Kumkufuru Mwenyezi Mungu

Utesi na wazazi wawili.

Kusengenya.

Kutia fitina.

Mwisho

Enyi wa Waislamu fanyeni haraka kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kufanya vitendo vyema. Mwenyezi Mungu Atuepushe na moto na adhabu yake na Atuingize peponi na Atujaalie ni katika wenye kusikia mema tuyafuate na Atuoneshe batili tuweze kuiepuka.





Vitambulisho: