islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


ZAKA ZA FITRI NA SWALA YA IDDI KATIKA UISLAMU


11257
wasifu
Utajo wa Mwenyezi Mngu kwa kiwiliwili ni kama maji kwa samaki. Samaki huwa vipi akiwa nje ya maji? Dini Ya mila iliyolingana sawa umemhimiza Muislamu afungamane na Mola wake, ili dhamiri yake iwe hai, nafsi yake isafishike, moyo wake utohirike na ajipatie kutoka Kwake msaada na taufiki. Kwa hivyo ymekuja kwenye Teremsho la Qur'ani liliothibitishwa na Sunna ya Mtume iliyotakata yenye kuvutia kumtaja Mwenyezi Mngu, Aliyetukuka na kushinda, kwa wingi katika kila hali, na kuwekea kila wakati na hali Utajo (wa Mwenyezi Mngu) wake.
Khutba ya

Allah (Subhaanahu wa Taala) ametuwekea zaka za fitri kwa hikma ya kuwa ni kafara pindi unapopatikana upungufu katika saumu ya Muislamu katika Mwezi wa Ramadhani. Na hakika hakuna binadamu mkamilifu. Na Iddi imewekwa ili kuonyesha kuwa Uislamu unazingatia maumbile ya binadamu, kwani binadamu huwa anapenda kuwa na wakati wa kusherehekea, kwa ajili hiyo ndio ikawekwa Iddi mbili ili ziwe sherehe zetu zimefungamana na ibada.

Kubainisha Maana ya Zaka za Fitri na Hukumu yake.

Ni nini maana ya zaka za fitri? Kabla ya kueleza hilo, napenda kuwakumbusha waja wa Allah ya kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni mgeni mtukufu aliyetujilia na amekurubia kuondoka. Inatakikana tupatilize siku zillizobakia kwa wingi wa toba na amali njema huenda Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) akaziunganisha amali zetu.

Enyi waja wa Allah, Mwisho wa mwezi huu mtukufu kuna amali tukufu zenye kuzidisha imani na kukamilisha ibada zetu, na amali hizo ni; zakatul fitri, takbira na swala ya iddi. Na zakatul fitri ni sadaka ambayo inapasa kwa sababu ya kufungua mwezi wa Ramadhani, na hakika imetambuliwa zaka za fitri kuwa ni swadaka ya wajibu, kwa hivyo ndio tunaiita zaka za fitri sadakatul fitri. Sasa twende katika kueleza hukumu ya zaka za fitri na dalili ya kuwekwa ibada hii.

Wanazuoni wa fiq’hi wameafikiana ya kuwa zaka za fitri inampasa kila Muislamu mwenye uwezo. Na dalili ni hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar asema katika mafhuum ya maneno yake: Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amefaradhishia watu inapomalizika Ramadhani kutoa pishi ya tende au pishi ya ngano, na hilo ni kwa kila Muislamu, awe muungwana au mtumwa, mume au mke”. Amepokea hadithi hii Bukhari.

Hikma ya kuwekwa Zaka za Fitri

Ni muhimu Muislamu kujua hikma ya zaka za fitri, hikma ya zaka za fitri ni mambo mawili :-

 

Hikma ya kwanza ni kuwa inatwahirisha saumu ya mwenye kufunga. Kwani binadamu kwa ubinadamu wake anaweza kufanya mambo ya kumpunguzia thawabu, basi hapo ndipo inapokuja nafasi ya zaka za fitri. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ametuambia katika hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Abbas katika maana ya hadithi: [Zaka za fitri ni twahara ya mwenye kufunga kutokana na upuuzi na maneno machafu, na ni chakula kuwalisha maskini]. Imepokewa na Abu Daud.

Hikma ya pili ni kuwakunjua mafukara na maskini na kuingiza furaha nyoyoni mwao.

Masharti ya kutoa Zaka za Fitri

Zaka za Fitri ina masharti yake :-

Sharti ya kwanza ni kuwa Muislamu. Kafiri si wajibu juu yake hata kama ana jamaa zake Waislamu ambao ni wajibu kwake kuwalisha.

Sharti ya pili ni mtu kuwa huru sio mtumwa. Kwani Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ametuambia: “ Watekelezeeni (zakatul fitri) kila huru na watumwa mnaowalisha”.

Sharti ya tatu ni uwezo wa kimali nao ni kuwa na chakula cha siku moja na usiku wake.

Sharti ya nne ni kuingia wakati, nao ni kutwa jua la siku ya Iddi mwisho wa mwezi wa Ramadhani. Na mwisho wa wakati wake ni baada ya kuswali iddi. Na mtu inafaa aanze kujitolea yeye mwenyewe kwanza kisha amtolee anayepaswa kumlisha. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). ametuambia katika maana ya Hadithi : [Jianzie na nafsi yako kisha unayemlisha].

Kiwango cha Zaka za Fitri na Vipimo vya Kisasa

Kiwango cha zaka za fitri ni pishi moja ya ngano au wimbi au zabibu au chakula chochote ambacho ni chenye kutumika sana mjini. Na pishi kwa kipimo cha kisasa ni kilo 2 na gramu 176. Ibnu ‘Umar amepokea hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), ya kuwa alifaradhisha zaka za fitri pishi ya mtama.

Na wanazuoni wa fiq’hi wa madhehebu ya hanafi waliporuhusu kutoa thamani ya kiwango cha chakula kinachopasa kutolewa ni kwa kuzingatia makusudio yaliyokusudiwa katika kufaradhishwa zaka, nayo ni kuwakidhia maskini haja zao katika siku hiyo ya iddi. Mu’adh amekubali kutoa thamani kwani ndio maslahi ya mafukara. Na Ibnu Taimiyya amesema hakuna ubaya wa kutoa thamani.

Khutba ya pili

Iddi katika Uislamu yakusanya Maana na Manufaa Makubwa

Kuna akida ambayo ni safi na ni kupiga takbira na dua na kunyenyekea bila ya kumshirikisha Mola, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), katika maana ya Aya:

(وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّهِ أَحَدًا) [الجن: 18]

{{Hakika Misikiti yote ni ya Mwenyezi Mungu, basi msiabudu yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu}}.

Na iddi, kuna kubainisha hukmu za Mwenyezi Mungu kwa kudhihirisha Alama za kiislamu. Na katika khutba kuna kufafanua hukumu za kiislamu kama vile kusubiri, kusamehe na kuondosha chuki katika nyoyo, na kuonyesha uhusiano mwema baina ya Waislamu. Kama alivyosema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) katika maana ya hadithi: [Watoshelezeni katika siku hii ya leo (yaani mafukara)]. Imepokewa na Daaraqutni kutoka kwa Ibnu Umar.

Baadhi ya Hukmu zinazopatikana katika Siku ya Iddi

kumtukuza Mola wakati tukikamilisha hesabu. Allah (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

فقال تعالى: (وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ) [البقرة: 185]

{{Ili mkamilishe hisabu na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwaongoza, na hakika mutamshukuru}}. Na kumeamrishwa hata wanawali na wenye hedhi watoke wapate kushirikiana na Waumuni wenzao katika dua. Kama hadithi iliyopokewa na Ummu ‘Atia.

Ni sunna kula tende au chochote katika iddil fitri kabla ya kwenda kuswali. Kama alivyoeleza Anas sunna hii ya Mtume. Na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ametuambia, katika maana ya Aya:

قال الله عز وجل): لقد كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآَخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا ) [الأحزاب: 21]

{{Hakika mna kielezo chema kwa Mtume wa Allah kwa mwenye kumtarajia Allah na siku ya mwisho na akamtaja Mwenyezi Mungu sana}}.

Mwisho

Tumeona kama ilivyo tangulia ya kuwa idd ni kuchunga maumbile ya binadamu, na zaka ni kuchunga maslahi ya mafukara na wasiojiweza na pia kurekebisha makosa madogo madogo ambayo huenda binadamu asiye weza kuepukana nayo.





Vitambulisho: