islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


swala ya kupatikana mwezi na jua


9499
wasifu
Jua na Mwezi ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu (SW) hupatw kwa uwezo wake,na kuenyesha nguvu za mwenyezi mungu kwa viumbe vyake, ili warejee kwake na watubie maasia waliyoyafanya. Na amewawekea kwa huko kupatwa jua au mwezi Swala ili wapate kurudi kwa Mwenyezi Mungu (SW) , waombe msada kwake awaondolee balaa hiyo.
Khutba ya

Usiku na mchana kupishana ni miujiza ya Allâh ili mwanaadamu anufaike nayo, na Akajaalia iwe chini ya utumishi wake. Hakuna anayeweza kukhalifu kanuni ya mwendo wa jua na mwezi isipokuwa Allâh (Subhaanahu wa Taala) Peke Yake. Sababu za kimaumbile, Waumini na makafiri wote wanaikubali. Sababu za Sharia, Waumini wanazikubali na makafiri wanazikanusha. Na dalili ni Kauli ya Allâh (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): وَمِنْ آَيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ )[فصلت: 37] {{Na katika alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi; basi msilisujudie jua wala mwezi; bali msujudieni Allâh Aliyeviumba ikiwa nyinyi mnabuabudu Yeye}}. Na Kauli Yake (Subhaanahu wa Taala):

وقوله :(وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ) [إبراهيم: 32] {{Na (Allâh) Akafanya iwatumikieni majahazi yanayopita baharini kwa Amri Yake, na Akaifanya mito iwatumikie}}.

Na Kauli Yake Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): وَآَتَاكُمْ مِنْ كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ وَإِنْ تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّهِ لَا تُحْصُوهَا إِنَّ الْإِنْسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ) [إبراهيم: 34]

{{Na Akawapa kila mlichomuomba. Na mkihisabu neema za Allâh hamuwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema}}.

Allah (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

قال تعالى :(وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ )[يس: 38]

{{Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua}}.

Allah (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

قال تعالى :(لَا الشَّمْسُ يَنْبَغِي لَهَا أَنْ تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ) [يس: 40]

{{Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao}}.

Abu Musa amesimulia: “Jua lilipatwa katika zama za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), akasimama huku akiwa amefazaika isije ikawa Qiyama kimesimama, akaenda Msikitini akasimama akiswali Swala yenye kisimamo kirefu, rukuu na sijda ndefu mno ambapo sijamuonapo akifanya hivyo katika Swala yoyote ile. Kisha akasema: [Alama hizi zinazotumwa na Allâh, huwa haziwi ni kwa kufa yeyote wala kuwa hai, bali Allah Anazituma Akiwahofisha waja Wake. Mtakapoona alama yoyote katika hizo, kimbilieni kumtaja Allah (Subhaanahu wa Taala), kumuomba dua na kumuomba istighfari]. Imepokewa na Muslim.

Kupatwa jua ni onyo la Mola juu ya kuepuka Sharia Yake. Mifano ya kukhalifu mafundisho ya Uislamu.

Allâh (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

قال تعالى): وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَى ظَهْرِهَا مِنْ دَابَّةٍ وَلَكِنْ يُؤَخِّرُهُمْ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا ) [فاطر: 45]

{{Na lau Allâh Angeliwachukulia watu kwa waliyoyachuma, basi Asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye Anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Allah ni Mwenye kuwaona waja Wake}}.

Jabir bin ’Abdullah Amehadithia: “Jua lilipatwa katika zama za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) siku yenye joto kali, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akawaswalisha Maswahaba zake, akarefusha kisimamo mpaka wakawa wakianguka, kisha akarukuu kitambo kirefu, akaitadili kitambo kirefu, akarukuu (tena) kitambo kirefu, akaitadili kitambo kirefu kisha akasujudu sijida mbili, akasujudu sijida mbili, kisha akasimama, akafanya kama alivyofanya mara ya kwanza. Ilikuwa ni Swala yenye rukuu nne na sijda nne. Nimeonyeshwa kila mahala mtakapoingia. Nikaonyeshwa Pepo, hata lau kama ningalichukua kichala (cha matunda) ningaliweza kukichukua. Nikaonyeshwa moto, nikamuona mwanamke wa Kiisraeli akiadhibiwa kwa sababu ya kumfungia paka ambaye hakumlisha wala hakumuacha aende akale vijidudu vya ardhini. Nikamuona Abu Thumama akiziburuta chango zake (matumbo) motoni. Watu walikuwa wakisema kuwa jua na mwezi havipatwi la kwa sababu ya kufa mtu mkubwa. Lakini hizo ni alama mbili za Allah Anawaonyesha, vitakaposhikwa, swalini mpaka viachwe.” Muslim.

Enyi umati wa Muhammad! Hakuna mwenye ghera kuliko Allah (Subhaanahu wa Taala) kumuona mja wake akizini, au mjakazi wake akizini. Enyi umati wa Muhammad! Lau mngalijua ninachokijua, mngalicheka kidogo na mkalia sana. Naapa kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), tangu niliposimama kuswali, niliona mutakayokutana nayo katika mambo ya dunia na Akhera yenu, hakuna ambacho sikukiona. Nimeyaona yote katika makamu yangu haya hata Pepo na moto. Nimeuona moto ukijitafuna wenyewe, sijaona mandhari ya kufazaisha kama leo. Nimemuona ’Amru bin Lahyi al-Khuzaiy akiburuta chango zake.

Nikamuona mwanamke akiadhibiwa kwa sababu ya paka, alimfungia wala hakumpa chakula wala hakumuacha aende akale vijidudu vya ardhini. Nimewaona jinsi mtakavyopewa mtihani makaburini mwenu, kama ule mtihani wa Dajjali atakapomjia mmoja wenu. Mtu ataulizwa: “ Mtu huyu unamjua vipi?” Muumini au mwenye yakini atasema: “ Ni Muhammad Mtume wa Allah, Alitujia na ubainifu na uongofu, tukamjibu, tukamuamini na tukamfuata.” hapo ataambiwa: “Lala ukiwa mwema. Tulikuwa tukijua kuwa ulikuwa ni mwenye yakini. Ama mnafiki au mwenye shaka, atasema: Simjui, niliwasikia watu wakisema kitu na mimi nikakisema!.

Khutba ya pili

Sharia ya Swala ya kupatwa Jua au Mwezi

Kuongezea dalili zilizotangulia, nitatoa dalili ya Hadithi ya Hudhaifa, amesema: “Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alikuwa anapofazaishwa na jambo, huswali.” Ibnu Jarir. Alqama amesema: “Mnapofazaishwa na vimondo vya mbinguni, kimbilieni kuswali”. Ibnu Abi Shaibah.

Namna ya kuswali Swala ya Kupatwa Jua au Mwezi

Abdur-Rahman bin Samurah amehadithia: “Nilipokuwa nikirusha mishale yangu – katika zama za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) mara jua likapatwa, nikaitupa. Nikasema kuwa nitamtazama Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) atakavyofanya katika hali ya kupatwa jua leo. Nilipofika kwake nilimuona akiinua mikono yake, akipiga Takbira na akisema : [Laa ilaaha illallah] mpaka jua likaachwa, akasoma Sura mbili na akaswali rakaa mbili”. Muslim. Abubakar amesema: “Jua lilipatwa katika zama za Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), akaswali rakaa mbili]. Bukhary.

Na Hadith ya ’Aisha amesema: [Jua lilipatwa wakati wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Mtume akasimama akawaswalisha watu. Akarefusha kisimamo, kisha akarukuu, akairefusha rukuu, halafu akasimama, akarefusha kisimamo – chini ya kisimamo cha kwanza - kisha akarukuu, akairefusha rukuu – chini ya rukuu ya kwanza – halafu akasujudu, akairefusha sijda. Kisha akafanya katika rakaa nyingine mfano wa alivyofanya katika rakaa ya kwanza. Halafu akamaliza na jua lilikuwa limeshaachwa (limeshadhihiri). Akaanza kuwahutubia watu. Akamshukuru Allâh na kumsifu, baadae akasema: “Hakika jua na mwezi ni alama miongoni mwa alama zenye kujulisha Uwezo na Umoja wa Allâh. Navyo havipatwi kwa kufariki yoyote wala uhai wa yoyote. Mtakapoona hivyo, muombeni Allah, mupige Takbira musali na mutoe sadaka. “Kisha akasema: “Enyi umati wa Muhammad! Naapa kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), hakuna mwenye ghera kumshinda Allah, kwa hivyo Ame haramisha zina kwa waja Wake; mwanamume au mwanamke. Enyi umati wa Muhammad! Naapa kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), lau mnayajua ninayoyajua, mngalicheka kidogo na mukalia sana!”. Katika lafdhi nyingine imesema: “ Akakamilisha rakaa nne na sijda nne].

Mdugu Waislamu, mafundisho ya Mtume yako wazi kabisa kuhusu suala la kupatwa jua au mwezi. Jukumu letu ni kufuta sunna ya Mtume kwa kutekeleza swala ya kupatwa jua au mwezi. Na tuachani itikadi mbaya za kimila juu ya matukio kama haya.

Mwisho

Ndugu katika imani na kuusieni kurudi kwa Allah (Subhaanahu wa Taala), kuacha kutenda dhambi na kuwafanyia uadilifu raia. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى): يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحًا عَسَى رَبُّكُمْ أَنْ يُكَفِّرَ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آَمَنُوا مَعَهُ نُورُهُمْ يَسْعَى بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ) [التحريم: 8]

{{Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allah toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi Akawafutia maovu yenu na Akawaingiza katika Pepo ambazo inapita mito kati yake, siku ambayo Allah Hatamdhalilisha Nabii na walioamini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu}}.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atuhifadhi na Atuepushe na kila shida za ulimwengu na Atujalie miongoni mwa waja wake watakao ingia peponi pamoja na Mtume Muhammad.





Vitambulisho: