islamkingdomface islamkingdomtwitte islamkingdominstagram islamkingdompinterest islamkingdomtumblr islamkingdomreddit islamkingdomvk


ATHARI YA MADHAMBI KATIKA MAISHA YA MWANADAMU


7477
wasifu
madhambi na masia yana athari kwa mtu anapo muasi mwenyezi mungu,kama vile twaa na ibada inavyo kuwa na athari kwa anae fanya mema.na mtume s.a.w ametuelezea kuwa mtu anapo fanya dhambi huingia katika moyo wake dowa leusi,na kila anapo fanya dhambi huingia dowa mpaka moyo wote ukawa mweusi,wakati huo huwa hasiki mema wala kuadhirika na mawaidha
Khutba ya

Himidi zote na shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu alieumba Mbingu na Ardhi akaumba na binadamu kwa malengo ya kumuabudu yeye peke yake. Aliyeweka Twaa na Maasia, mwenye kumtii ataingia peponi na mwenye kumwasi ataingia motoni. Swala na Salamu zimshukie kipendi chetu Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam), Yeye na Aali zake na Swahaba zake wote.

Waja wa Mwenyezi Mungu, na wausia pamoja na kujiusia mimi mwenyewe kumcha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Muogopeni Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), na Kufuata mwenendo wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na waja wema waliotangulia.

Waja wa Mwenyezi Mungu, hakika maasia yana athari mbaya kwa mtu mmoja bali kwa mujitamaa wote. Na wala hakuna shaka ya kwamba maasia wanayo fanya watu usiku na mchana athari ambayo inaangamiza mtu mmoja na jamii yote na maisha yote. Kwa hivyo, nguzo ya maisha na kutengenea kwa maisha ni katika twaa na kwa msimamo juu ya amri ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kufuata sharia ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyo safi. Na kujiepusha na twaa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ni kumfuata shetani.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى : (فَبِمَا نَقْضِهِمْ مِيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَنْ مَوَاضِعِهِ وَنَسُوا حَظًّا مِمَّا ذُكِّرُوا بِهِ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَى خَائِنَةٍ مِنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِنْهُمْ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ )[المائدة: 13]

{{Basi sababu ya kuvunja ahadi kwao tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao ngumu, wanabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu wameacha sehemu ya yale waliokumbushwa na utaendelea kupata habari zao basi wasamehe na waache hakika Mwenyezi Mungu anawapenda watu wema}} [Al-Maidah : 13].

Athari ya Maasia

- Nyoyo kuwa ngumu

- Kubadilisha maneno ya Allah (Subhaanahu wa Taala) bila ya kujali

- Raana ndani ya moyo nayo moyo kuwa mweusi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): (Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao kwa maovu waliyoyachuma). Inaonyesha ya kwamba maasia yana athari mbaya sana, nazo ni kuwa nyeusi nyoyo za watu wenye kuasi hapo huwa hazijui mema wala mabaya, haziamrishi mema wala hazikatazi mabaya.

- Kusahau kitabu cha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Na tunaposahau maagizo ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ni kuishi maisha mabaya. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

وقال): وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى124 قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَى وَقَدْ كُنْتُ بَصِيرًا 125قَالَ كَذَلِكَ أَتَتْكَ آَيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا وَكَذَلِكَ الْيَوْمَ تُنْسَى 126وَكَذَلِكَ نَجْزِي مَنْ أَسْرَفَ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِآَيَاتِ رَبِّهِ وَلَعَذَابُ الْآَخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبْقَى.127)

{{Mwenye kupa mgongo utajo wangu hakika tutampa maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya kiyama akiwa kipofu}}.

- Athari kubwa ya maasia na iliyo khatari ni ugomvi baina ya mja na Mola wake.

- kuwa mzito kumtii Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

- Kukosekana hifadhi ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

- Kusalitiwa na maadui na kuwa dhaifu mbele ya adui pamoja na kuondolewa utisho kutoka katika nyoyo za maadui

- Kudhihiri njaa na kuondoshwa baraka katika riziki.

Khutba ya pili

Shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) alie mwingi wa rehema ambae hakuzaa wala hakuzaliwa Mwenye nguvu na uwezo wa kila kitu anafanya analo litaka haulizwi analolifanya na nyinyi mtanaulizwa. Anafanya alitakalo kwa kusema kuwa lina kuwa.

Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema na amani kipenzi chako Mtume Muhammad kama ulivyo mrehemu Mtume Ibrahimu na umbariki Mtume Muhammad kama ulivyo mbariki Nabii Ibrahim kwa viumbe. Wewe ni Mwenye kushukuriwa .

Enyi waislamu, hakika anae taka amani ya ulimwenguni na akhera ni ajilazimishe na kumtii Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na Mtume wake.

قال تعالى) : وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ) [الأحزاب: 71]

{{Mwenye kumtwi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hakika amefaulu kukubwa}}. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amefunganisha kufaulu kwa mwanadamu ni kushikamana na twaa yake, na kufeli kwa mwanadamu ni kumuasi Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Kwa hivyo, tushikamane na twaa ya Mwenyezi Mungu ili tupate kufaulu ulimwenguni na kesho siku ya kiyama. Kisha Mwenyezi Mungu Akaamrishwa kukimbilia kwake kwa kumuomba msamaha wake.

قال تعالى) : وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )[النور: 31]

{Rudini kwa Mwenyezi Mungu nyote ni waisilamu huenda mukafaulu}. katika Aya hii Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Anatuonesha ya kwamba tufanye haraka kurudi kwake, tupate mafanikio ya ulimwenguni na akhera.

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, jueni ya kwamba kitakacho waokowa nyinyi na adhabu ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) ni kuamrisha mema na kukataza mabaya kama alivyo elezea kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Imepokewa na Hudhayfa mtoto wa Yamani (Radhiya Llahu ‘anhu), Akipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [ Naapa kwa Mwenyezi Mungu ambae nafsi yangu iko mikononi mwake mtaamrishana mema na mtakatazana mabaya au tutawaletea nyinyi adhabu kali, kisha mtamuomba Mwenyezi Mungu, na hatawajibu]. Imetolewa na Tirrmidhi. Hadithi hii inatuonyesha ya kuwa kufaulu kwetu inatokana na kuamrisha mema na kukatazana mabaya la sivyo, basi hatuna kufaulu hata maombi yetu hayatakubaliwa.

Masharti ya Kurudi kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

Kurudi kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kuna masharti yake. Wanavyuoni wametaja masharti hayo, nayo ni kama ifuatavyo:

Ni kujuta kwa uliyo ya fanya yote

Kuweka nia kuto rudiya madhambi uliyo yafanya katika baki ya umri wako

Kuacha maasiya yote.

Kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa wakati wake. yaani kabla juwa halijatoka upande wa kuchwa.

Mwisho

Enyi Waisilamu rudi kwa Mwenyezi Mungu mupate mafanikio mema ya ulimwenguni na akhera na muepukane na kumuasi Mwenyezi Mungu. Kwani hakupatikani mafanikio bora pamoja na kumuasi Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, tushikamane na twaa ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kufuata njia na mafundisho ya Mtume Muhammed (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).

Mwenyezi Mungu atujaalie ni wenye kushikamana na twaa yake na atupe mafaniko bora ya ulimwenguni na akhera atupe mwisho mwema tukutane na Mwenyezi Mungu kwa salama atujaalie ni wenye kusikia mema pamoja na kuyafuata.





Vitambulisho: